kama ni mapenzi
ya kuniudhi kila saa, ya kunifanya mi kulia
na kama huridhiki
na mbona hujasema, ili niweze rekebisha
ilifaa ni mambo shwari
nikiamini u kwangu, na kukusifu kwa wazazi
hujali tena hisia zangu
sijui tunapokwenda, lakini najua tulipotoka
kutoka sitoki nimetekwa nyara
kukuwacha siwezi kibarua ngumu
nashindwa ni nini ntafanya uridhike
nimetekwa ndani, mtandao wa mapenzi
basi nakuomba, uniteke tu bila mateso
tazama, nimezama, ndani ya bahari, la penzi lako
siwezi, kusonga mbele, kurudi nyuma, sijielewi
haya mapenzi ya fujo hayafai
kama wanipenda, jaribu kunipa raha
mi nashangaa, watu wakisema
eti tunapendana, japo tunazozana
ni vizuri mami, kumba kuwa na siri
lakini jaribu, tusuluhishe
bila hivyo, itakuwa mteso
wa kuigiza, kwenye mambo bandia
mimi sitaki, mambo ya kujifanya
ati tunapendana, tena tunatesana
nimejaribu sana kujitoa ndani
kila nikipanga napangua mwenyewe
natamani sana ungeelewa hivyo
mimi mateka, mimi pumbavu (mabusu), wa penzi lako
nieleze ni lini ntakuwa huru
tazama, nimezama...
jaribu baby...mambo, ya kunifanya kumbafu haifai
mambo yo yo yo yo yo...haifai, jaribu baby, tusuluhishe
nimejaribu sana kujitoa ndani...
tazama, nimezama...
haya mapenzi ya fujo hayafai
kama wanipenda, jaribu kunipa raha...(ad libitum)